Maisha
Ndani ya
Maji

In partnership with

Matumbawe yanakaa katika chini ya asilimia 1 ya eneo la bahari …

… ilhali ndiyo nyumbani kwa zaidi ya asilimia 25 ya wanyama wa majini.

Shughuli za binadamu na sayari kupata joto zinaharibu mazingira haya ya aina yake na yaliyo dhaifu haraka sana.

Hadithi hii ni msururu kutoka UNEP unaoonyesha jinsi wanadamu wanaweza kuishi kwa pamoja na mazingira asili kwenye sayari isiyo na uchafuzi wa mazingira na ambapo hali ya hewa ni thabiti.

Hadithi zaidi kutoka kwenye misururu

Hali ya Miamba Matumbawe ya Dunia: 2020 ni ripoti ya Global Coral Reef Monitoring Network (GCRMN), mtandao wa kimaitaifa wa Mpango wa Kimataifa kuhusu Miamba Matumbawe (ICRI). Matokeo yake yanaonyesha kwamba kati ya 2009 na 2018 kulikuwa na hasara ya takriban asilimia 14 ya matumbawe kutoka kwa miamba tumbawe iliyo duniani hii ikisababishwa kimsingi na matukio ya kupaushwa yanayotokea mara kwa mara na katika eneo pana. Kwa hayo yote, takriban kilomita mraba 11,700ya matumbawe magumu, hii ikiwa ni zaidi ya matumbawe yote yaliyopo kwenye miamba matumbawe nchini Australia, yalipotea.

Ripoti hiyo inatoa taswira ya miongo minne ya kudidimia kwa matumbawe, ongezeko la upaushaji na idadi ya juu ya miani, ambayo ni ishara ya kudidimia kwa afya ya miamba matumbawe. Hata hivyo, ripoti hiyo pia inafichua uwezo wa kipekee wa miamba matumbawe kurejea ikiwa haitatatizwa na matishio ya ndani na ya kimataifa. Matokeo yote mawili yanapaswa kuchochea hatua ya haraka kuchukuliwa. Ingawa miamba matumbawe yanasalia kufichika yasionekane na watu, afya yao lazima ipewe kipaumbele katika jitihada za kimazingira na michakato ya kufanya uamuzi.

Ripoti hii:

Ndiyo ya kwanza katika muda wa miaka 13

Inachunguza hali ya miamba matumbawe duniani katika miaka 40 iliyopita.

Inawakilisha kazi ya zaidi ya wanasayansi 300kutoka jamii ya wanasayansi kote duniani

Ina msingi wake kwenye setidata ya duniani inayojumuisha takribani maoni milioni 2

Kutoka zaidi ya vituo 12,000

Katika nchi 73

Kote maeneo 10 ya GCRMN

Abstract watercolor illustration of a group of corals

Matumbawe Katika Hatari ya …

Ndani ya eneo la bahari pamefichwa mandhari yenye mguso na rangi anuai ya miamba ya matumbawe. Miji hii inayobadilika ya ndani ya maji inasaidia maisha ya aina 800 tofauti ya matumbawe magumu na ni nyumbani kwa zaidi ya asilimia 25 ya wanyama wa majini. Miamba matumbawe hukua kwa muda wa maelfu ya miaka kutokana na mamilioni ya kila chembe kidogo cha polyps za matumbawe ambazo hutoa madini ya calcium carbonate exoskeletons ili kuunda miamba ya matumbawe magumu ambayo ndiyo msingi wa miamba matumbawe. Matumbawe laini hujikinga na kuyumbayumba miongoni mwa milima ya miamba ya matumbawe magumu hivyo kutoa makao ya ziada kwa samaki, konokono na viumbe vingine vya majini.

Miamba matumbawe ina maisha ndani yake. Hakika, imebeba maisha ya aina nyingi zaidi ya viumbe katika mazingira yoyote duniani, hii ikiifanya kuwa mazingira changamano kibayolojia na yenye thamani katika sayari hii. Mazingira haya ya kipekee yapo katika kila hali ya hewa na yanasaidia zaidi ya watu bilioni 1 katika huduma zao za thamani za mazingira.

Hata hivyo, matumbawe yanakumbwa na janga la uwezekano wa kutoweka kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na matishio mengine ya ndani na vyanzo vya matatizo.

Udhaifu wa miamba matumbawe kwa joto la baharini unaifanya kuwa mojawapo ya mazingira dhaifu zaidi kwa mabadiliko ya hali ya hewa.

Nyuzijoto za juu baharini — na mawimbi ya joto baharini — ndiyo sababu kuu za kudidimia na kupaushwa kwa matumbawe.

Maji yanapopata kiasi cha juu cha joto kwa matumbawe, matumbawe hudondoa miani yake midogo yenye rangi nyingi na kubadilika kuwa meupe.

Baadhi ya matumbawe “humetameta” kwa kuzalisha safu ya ulinzi ya rangi za neoni kiasilia kabla ya kupauka.

Ikiwa matukio ya kupauka yataendelea kwa muda mrefu au kufanyika mara nyingi bila kupata muda wa kutosha wa kurejea hali ya kawaida, vifo vingi vya matumbawe vinaweza kutokea, hii ikiwa na athari kwa miamba matumbawe.

Kupauka kunaweza kudhaniwa kuwa namna ya ‘ishara ya mapema ya hatari’ kwa sababu kunaonyesha jinsi matumbawe yanavyotishiwa na hali hatari na zinazoweza kusababisha vifo vyao.

Kulingana na Ripoti ya GCRMN, Hali ya Miamba Matumbawe ya Dunia: ya 2020, kumekuwa na hali ya kupungua kwa idadi ya matumbawe magumu tangu 2010. Athari mbaya zaidi imetokea Asia Kusini, Australia, Pacific, Asia Mashariki, Magharibi wa Bahari Hindi, Ghuba na Ghuba ya Oman.

Hard coral coverundefined25%25%26%26%27%27%28%28%28%29%30%30%31%31%32%32%33%33%34%34%35%35%36%36%37%37%38%38%39%39%40%40%41%41%19801985199019952000200520102015

​​Kumbuka: Maeneo yaliyotiwa rangi nyuma ya line yanawakilisha 80% and 95% credible intervals —au jinsi wachapishaji walivyo na uhakika kuhusu makadirio yao.

Tangu 2010, kiasi cha miani kwenye miamba ya matumbawe duniani imeongezeka kwa takribani asilimia 20, hii ikiashiria kupungua kwa idadi ya matumbawe magumu kwa kipindi hiki cha wakati.

Algae coverundefined6%7%8%9%10%11%12%13%14%15%16%17%18%19%20%21%22%23%24%25%26%1988199019921994199619982000200220042006200820102012201420162018

​​Kumbuka: Maeneo yaliyotiwa rangi nyuma ya line yanawakilisha 80% and 95% credible intervals —au jinsi wachapishaji walivyo na uhakika kuhusu makadirio yao.

Mabadiliko kutoka miamba inayotawaliwa na matumbawe hadi inayotawaliwa na miani husababisha kupungua kwa hali changamano ya usanifu na uadilifu wa kimuundo wa makao haya. Kutokana na hayo, inapungua katika kuwa anuai kibayolojia na kutoa bidhaa na huduma chache zaidi kwa wanadamu.

Mchakato huo uko wazi katika mwendo huu wa majira: huku matumbawe yakipauka

miani inachukua nafasi yake.

Ripoti ya UNEP ya 2020 Projections of Future Coral Bleaching inasema kwamba matukio ya kupauka kote duniani yanaweza kuwa ya kawaida katika miongo ijayo kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Ripoti hiyo inakadiria kwamba isipokuwa tupunguze haraka ufachuzi wa hewa kupitia kuachilia kaboni hewani, miamba matumbawe yote kote duniani itapauka kufikia mwishoni mwa karne hii. Kufikia 2034, upaushaji mbaya zaidi unatarajiwa kufanyika kila mwaka. Wakati huu, suluhisho haliwezi kupatikana isipokuwa ikiwa matumbawe yanaweza kuanza kunawiri katika hali ya joto jingi.

Matumbawe siyo spishi pekee zilizo hatarini katika ulimwengu wetu unaopata joto. Zaidi ya spishi milioni 1 za mimea na wanyama huenda zikatoweka katika miongo ijayo, hii ikihatarisha ustawi na maisha ya wanadamu, yasema ripoti ya Intergovernmental Science-Policy Platform on Biodiversity and Ecosystem Services. Matumbawe, hata hivyo, yameonyesha ongezeko la haraka la hatari ya kutoweka kati ya spishi zote zilizotathminiwa na Uchunguzi wa Maisha Anuai Duniani. Athari ya bahari kupata tindi pamoja na joto jingi baharini na sababu za kindani, kama vile uvuvi kupita kiasi, uchafuzi utalii usioendelevu na usimamizi mbaya wa pwani, zinakuja pamoja kama dhoruba kali inayosukuma mazingira haya nyeti kutoweka.

Mwanga wa Matumaini

Licha ya tathmini hizi za kusikitisha, hatujapoteza matumaini kabisa kuhusiana na miamba ya matumbawe. Ina ustahimilivu wa juu na inaweza kurejea endapo hakuna uharibifu wa kiasi kikubwa.

Baada ya tukio la kupauka kwa matumbawe kwa wingi mwaka wa 1998, matumbawe magumu yalirejea na kufikia viwango vilivyokuwepo kabla ya 1998 ndani ya mwongo mmoja.

Mwaka wa 2019, licha ya kuongezeka kwa matukio ya kupauka, idadi ya matumbawe kwenye miamba ya dunia iliongezeka kwa asilimia 2. Wanasayansi pia wanatambua sehemu za makao ya matumbawe ambayo ni stahimilivu zaidi kwa mabadiliko ya hali ya hewa. Sehemu hizo zimepatikana kwenye miamba iliyo katika pwani ya nchi kama vile Kenya, Tanzania, Australia, Indonesia, Malaysia na India. Kutafuta na kujumuisha maeneo salama ya matumbawe au ‘refugia,’ kwenye mipango ya utunzi wa mazingira ni muhimu katika kuhakikisha mustakabali wa miamba matumbawe upo huku tukifanya kazi kukomesha na kubatilisha matishio ya sasa.

Tukikomesha na kurekebisha hali ya bahari kupata joto kupitia ushirikiano wa kiulimwengu, tunaipa miamba ya matumbawe fursa ya kurejea kutoka pabaya. Hata hivyo, itahitaji hatua yenye matamanio, ya haraka na iliyodhaminiwa vyema ya hali ya hewa na bahari ili kuokoa miamba matumbawe ya dunia.

Illustration of the different aspects of the economy where Corals are important

Kwa Nini Tunapaswa Kuchunga

Miamba matumbawe ni ya thamani kubwa, na umuhimu wake hauwezi kudunishwa.

Ingawa inakalia chini ya asilimia 1 ya eneo la bahari ...

… matumbawe ni msingi wa jamii nyingi za pwani, yakiwapa watu chakula, ulinzi dhidi ya dhoruba, dawa za kuokoa maisha …

… na kipato kutokana na utalii na uvuvi.

Miamba matumbawe inachangia dola bilioni $36 za Marekani katika sekta ya utalii kote ulimwenguni kila mwaka.

Pamoja na hayo, zaidi ya watu bilioni 1 wananufaika moja kwa moja na miamba ya matumbawe.

Manufaa ya kiuchumi ya miamba matumbawe yanakua au kufifia kwa kutegemea hali yao ya afya. Kurejesha matumbawe kunaweza kufungua mabilioni ya dola katika thamani ya kiuchumi, yasema Ripoti ya Uchumi ya Miamba Matumbawe kutoka UNEP, the Prince of Wales's International Sustainability Unit, the International Coral Reef Initiative na Trucost.

Ripoti hiyo ilipata kwamba utalii, maendeleo ya pwani na uvuvi wa kibiashara unaotegemea miamba matumbawe kila mwaka unatoa thamani ya Dola za Marekani bilioni $6.2 kule Mesoamerica na thamani ya Dola za Marekani bilioni $13.9 kwenye Coral Triangla. Miamba hii ikiendelea kudidimia katika mwongo ujao, thamani yao ya kila mwaka itashuka kwa asilimia 50 kule Mesoamerica na asilimia 16 kwenye Coral Triangle. Hata hivyo, miamba matumbawe hii inaweza kuzalisha Dola za Marekani bilioni $8.7 kila mwaka kule Mseoamerica na Dola za Marekani bilioni $16.5 kila mwaka katika Coral Triangle ikiwa miamba hii itafufuliwa kufikia 2030.

Abstract watercolor illustration of a group of corals

Manufaa Kando na ya Kiuchumi

Thamani ya miamba matumbawe yenye afya ni zaidi ya uchumi.

Miamba matumbawe yenye afya ndiyo mstari wa mbele kwa mamilioni ya viumbe katika pwani mbalimbali kote duniani. Inapunguza mawimbi ya nishati, ni vizuizi vya dhoruba, huzuia mimomonyoko mibaya na kuzuia mafuriko, hususan katika majimbo ya visiwa vidogo na mataifa yenye matumbawe. Miamba matumbawe inazingatiwa kama misitu ya bahari na makabati ya dawa ya karne ya 21. Siku zijazo, miamba matumbawe inaweza kuwakilisha ongezeko la vyanzo muhimu vya dawa kwa magonjwa mbalimbali (saratani ikiwemo), viziada vya lishe na bidhaa nyingine ya kibiashara. Hakika, uwezekano wa kupatikana kwa dawa mpya baharini, hususan miongoni mwa spichi za miamba matumbawe, huenda ukawezekana kwa mara 300-400 zaidi kuliko kupatikana kutoka kwenye mazingira ya ardhini.

Ikiwa umewahi kuogelea, kuogelea kwa kutumia magwanda maalum ya majini au kuruka majini, au kuchungulia tu baharini huku ukiwa umesimama bila viatu mchangani, unafahamu kwamba vigezo vingi vya bahari havihesabiki ila tu unaweza kukiri utulivu na mshangao uliopo. Lakini, muda umewadia wa kuchukua hatua kwa ajili ya bahari zetu na kuokoa miamba matumbawe ya dunia.

Sayansi Inaweza Kusaidia Kuokoa Matumbawe

Mwaka huu ni mwanzo wa Mwongo wa Umoja Mataifa wa Sayansi ya Bahari kwa Maendeleo Endelevu Mwongo wa Umoja wa Mataifa kuhusu Urejesho wa Mazingira.

Kampeni hizi zimeundwa ili kusaidia kulinda bahari zetu kupitia maendeleo ya kisayansi na kufufua mazingira ya sayari hii yanayodidimia.

Sayansi ni zana mahiri sana. Sayansi ilichangia kurekebishwa kwa tabaka la ozoni, ilisaidia utengezaji wa haraka wa chanjo za COVID-19, na inaweza kurekebisha kudidimia kwa bahari na miamba matumbawe. Sayansi pia ilikuwa msingi wa ripoti ya GCRMN The Status of Coral Reefs of the World: ya 2020, inayoonyesha kwamba mwaka wa 2019, eneo la bahari duniani lililo na matumbawe magumu kwa wastani kwenye miamba matumbawe ya dunia lilikuwa asilimia 29.5, ikilinganishwa na asilimia 32.3 la mwaka wa 1978. Eneo lenye matumbawe ni kipimo cha asilimia ya eneo la miamba matumbawe lililo na matumbawe magumu yanayojenga miamba.

Upana wa kila safuwima unawakilisha mgao wa miamba matumbawe iliyo ndani ya kila eneo.

Urefu wa sehemu ya manjano unawakilisha eneo la wastani lenye matumbawe magumu katika kila eneo mwaka wa 2019.

Mwaka wa 2019, eneo la dunia lililokuwa na matumbawe magumu kwa wastani lilikuwa asilimia 29.5.

Lakini eneo lililo na matumbawe linatofautiana kutoka eneo moja hadi jingine. Miamba matumbawe iliyo Pasifiki kwa wastani, ni karibu maradufu ya matumbawe kwenye Caribbean.

Pia, kila eneo linaonyesha matukio tofauti. Tazama jinsi eneo la wastani lenye matumbawe magumu limebadilika katika kila eneo kwa muda.

Bahari imechukua asilimia 70 ya eneo la Dunia, ila tunafahamu machache sana kuhusu yaliyomo chini yake.

Tunachofahamu ni kwamba kukabiliana na uharibifu wa miamba matumbawe kunahitaji mbinu ya ushirikiano wa wote. "Juhudi za matamanio na zilizoratibiwa za serikali, biashara na watu kote duniani zinaweza kuzuiwa na kurekebisha athari mbaya zaidi za uharibifu wa mazingira kwa kubadilisha mifumo muhimu, ikiwa ni pamoja na kawi, maji na chakula, ili matumizi yetu ya ardhi na bahari yawe endelevu zaidi," yasema ripoti ya Umoja wa Mataifa ya Making Peace with Nature. Mbinu mpya inamaanisha kuipa kipaumbele afya ya ulimwengu wetu asili katika kufanya maamuzi ili mifumo ya kijamii na kichumi ionyeshe na kudumisha thamani zao za ndani na za nje.

Abstract watercolor illustration of a group of corals

Je, Tunawezaje Kuleta Mabadiliko

Kati ya 2021-2022, viongozi wa kisiasa watahudhuria matukio ya kufanya maamuzi muhimu ya mustakabali wa miamba matumbawe.

Tukio la kwanza ni mkutano wa 15 wa Kongamano la Wanachama (CoP) wa Kongamano la Jamii Nyingi za Viumbe Kibiolojia (Oktoba 2021 na Aprili 2022)

Hapo, serikali za dunia zitaunda muundo wa jamii nyingi za viumbe duniani wa baada ya 2020, utakaotumika kama kundi la malengo ya dunia yanayoruhusu wanadamu kuishi pamoja na mazingira asili katika mwongo ujao.

Katika miaka miwili iliyopita, Mpango wa Kimataifa wa Miamba Matumbawe ushirikiano wa wanachama 93, ikijumuisha serikali, vikundi vya kijamii na raia na kampuni za sekta ya kibinafsi, umetoa mapendekezo ya kutunza miamba matumbawe. Msingi wa pendekezo: kuchukua hatua kuipa kipaumbele miamba matumbawe kunaweza kuzalisha manufaa ya Dola za Marekani trilioni $2.7, na kuchangia usalama, lishe, usalama wa kiuchumi, afya na ustawi wa zaidi ya watu bilioni 1. Pendekezo hilo, litakalowasilishwa katika Kongamano kuhusu Jamii Nyingi za Viumbe Kibiolojia, miito ya kutambuliwa kwa miamba matumbawe kama mazingira yaliyo hatarini zaidi na miito ya matumbwe kupewa kipaumbele ndani ya muundo wa kimataifa wa jamii nyingi za viumbe baada ya 2020. Inajumuisha viashiria kadhaa vya wazi vinavyokadiria afya, uadilifu na utendakazi wa miamba matumbawe, ikiwa ni pamoja na:

Abstract watercolor as an illustration for the the text below

Eneo Lenye Matumbawe — inatoa taswira ya afya ya jumla ya miamba matumbawe

Abstract watercolor as an illustration for the the text below

Ufikio wa Miamba Matumbawe — hubaini ikiwa eneo la mifumo ya miamba matumbawe inaongezeka au kupungua

Abstract watercolor as an illustration for the the text below

Uwepo wa Miani Minene na kufunikwa kwa vikundi muhimu — huashiria maisha ya miamba matumbawe, kuongezeka kwa miani kwenye miamba matumbawe kunaweza kuonyesha kudorora kwa maisha yao

Abstract watercolor as an illustration for the the text below

Upatikanaji wa Samaki na Uzito wa Viumbe Hai — unaakisi uzalishaji na uadilifu kiutendakazi wa miamba matumbawe

Abstract watercolor as an illustration for the the text below

Asilimia ya Miamba Matumbawe Iliyolindwa Ipasavyo — hukadiria kujitolea kulinda miamba matumbawe

Abstract watercolor as an illustration for the the text below

Kipimo cha Uchafuzi wa Pwani — kinaashiria athari za ubora wa maji katika maeneo ya pwani

Hatua ya pili kwa wafanya maamuzi ni mkutano wa 26 wa Kongamano la Wanachama wa Kongamano la Muundo wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa. Kongamano la mwaka huu kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa ni muhimu kwa mataifa kuendeleza Mkataba wa Paris kuhusu kupunguza utoaji wa gesi hewani ili kukomesha kupanda kwa joto la wastani duniani hadi chini ya 2° C.

Tunafahamu kinachopaswa kufanywa ili kuokoa miamba matumbawe ya Dunia: kutatua mabadiliko ya hali ya hewa duniani kwa dharura, huku tukipunguza sababu zingine za ndani zaidi za kimazingira kama vile kupunguza uvuvi kupita kiasi, uchafuzi wa maji machafu na mbolea, uchotaji wa mchanga na maendeleo katika pwani. Mikutano hii miwili ni nguzo katika kuendeleza na utekelezaji wa suluhisho linalofaa la janga linalokabili miamba matumbawe.

Lakini kulinda miamba matumbawe si kazi ya viongozi wa kisiasa pekee. Wewe pia unaweza kuonyesha viongozi hao kwamba unajali na unamakinikia kutetea kuwepo kwa mabadiliko ya haraka na yenye maana zaidi. Kampeni ya UNEP ya Glowing Glowing Gone Campaign inatoa mwito kwa ulinzi thabiti wa mazingira ya matumbawe na kutokuwepo kwa kaboni hewani kufikia 2050. Kampeni hiyo yenye kaulimbiu, "Na tuwe kizazi cha kwanza kuokoa mazingira mzima," inalenga kuipa motisha umma na vyombo vya habari kutoa sauti zao na kuwa mabalozi wa mabadiliko kwa kuchukua hatua za kupunguza athari zao wenyewe za kimazingira. Sayari yenye afya ina maana kuna watu wenye afya na afya ya sayari inategemea mustakabali wa miamba matumbawe.

Abstract watercolor illustration of a group of corals
Cover of the report

Download the report: The Status of Coral Reefs of the World: 2020

Embed our charts (from Datawrapper)

Additional resources